14 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Uwezo wa kuifunga Cranes mnao - Khatib
 
2008-05-14 09:48:01
By Somoe Ng\'itu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Muhammed Seif Khatib amewaambia wachezaji wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars kuwa wanauwezo wa kushinda mechi ya Jumamosi dhidi ya Uganda, The Cranes na kuipatia nchi furaha na heshima.

Mechi hiyo ni ya marudiano wakati mchezo wa kwanza uliofanyika Mei 3 kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Akizungumza jana kwenye kambi ya wachezaji hao iliyopo Msasani, jijini Dar es Salaam, Khatib alisema kuwa wachezaji walioko katika timu hiyo wana uwezo na uzoefu ambao waliupata katika mechi za makundi mwaka jana walipokuwa wanatafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizopita.

Khatib alisema kuwa viwango ambavyo vinaonyeshwa na wachezaji wa Stars ndio vinampa imani kubwa kuwa wanaweza kushinda katika mchezo huo na kusonga mbele kwenye mashindano hayo.

Aliongeza kuwa ushindi wa mechi hiyo utawaongezea nafasi wachezaji kwa kuweza kupata nafasi nzuri ya kuitwa katika timu za nje na hivyo kunufaika baada ya kufanya kazi nzuri.

Alisema kuwa hakuna ambacho kinaweza kukwamisha dhamira hiyo kwa sababu hivi sasa timu hiyo inapatiwa kila kinachohitajika kutokana na uongozi bora uliopo na fedha zinazotolewa na wadhamini wa timu hiyo tofauti na miaka ya nyuma ambapo posho na chakula cha kuhudumia kambi kilikuwa kikipatikana kwa tabu.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.