15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wanachama waafiki Kaduguda kusimamishwa
 
2008-05-15 08:48:22
By Somoe Ng\'itu

Wanachama wa klabu ya Simba ya jijini wameungana na viongozi wao kwa hatua waliochukua ya kumsimamisha katibu mkuu wao, Mwina Kaduguda kutokana na kutuhumiwa kwa utovu wa nidhamu alioufanya kwa nyakati mbalimbali na kufikia makosa 11.

Wakizungumza na gazeti hili jana kwenye makao makuu ya klabu yao, wanachama hao walisema kuwa Kamati ya Utendaji iliyokutana juzi na kuamua kumsimamisha kiongozi huyo haijakosea kwa sababu wao ndio wanafahamu utendaji wa kiongozi huyo kutokana na kuwa naye karibu.

Ramadhani Mohammed mwenye kadi namba 1611 alisema kuwa hadi kufikia maamuzi ya kusimamishwa kiongozi huyo na wenzake inaonyesha kuwa hayuko sahihi katika majukumu yake na hatua kali zaidi zitachukuliwa katika mkutano wa wanachama unaotarajiwa kufanyika mwezi Agosti endapo itabainika ni kweli alifanya makosa hayo anayotuhumiwa.

Mohammed alisem kuwa maamuzi hayo yasiishie kwa Kaduguda peke yake bali na kwa wengine watakaoenda kinyume ili kuhakikisha kuwa klabu inakuwa na amani katika kipindi hiki cha usajili.

``Kwa kifupi maamuzi waliyofanya ya kumsimamisha Kaduguda ni sahihi, kwa sababu klabu inahitaji kufanya mambo mengi hasa ukizingatia katika ligi Simba haijafanya vizuri na suala la usajili linakuja ambalo linahitaji ushirikiano,`` alisema Mohammed.

Naye Haruna Nazi alisema kuwa kilichofanywa na kamati hiyo ni sahihi kwa sababu klabu inahitaji kuwa na viongozi waadilifu na wala jambo hilo lisichukuliwe kama chanzo cha kuanzisha mgogoro wowote klabuni.

Juma Mnonji alisema maamuzi ya aina hiyo yasiishie kwa mtu mmoja bali wote ambao wanaonekana kuwa hawatimizi majukumu yao nao wachukuliwe hatua.

Hata hivyo, jana Kaduguda hakuweza kupatikana katika simu yake ya mkononi ili kuzungumzia tuhuma zinazomkabili.

Mwanachama mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Method Milanzi alisema kuwa viongozi wao hawajakosea kwa sababu Kaduguda alikuwa haeleweki katika maamuzi mbalimbali hata yale ambayo alishiriki kuyaamua katika vikao halali wanavyokutana.

Jambo lililoonyesha kuwakera zaidi viongozi wa Simba ni kutoleana kwa lugha chafu dhidi ya mmoja wa wafadhili wa klabu hiyo ambaye alikuwa anamlipa mshahara kocha huku pia akidaiwa kuchangia kujitoa kwa Dionis Malinzi.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.