15 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Stars wakabidhiwa bendera
 
2008-05-15 08:49:11
By Somoe Ng\'itu

Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo amesema kuwa timu yake inakabiliwa na changamoto kubwa katika mechi ya marudiano dhidi ya Uganda, The Cranes ambayo imepangwa kufanyika keshokutwa kwenye uwanja wa Nakivubo, jijini Kampala.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Maximo alisema kuwa anafahamu kuwa mchezo huo utakuwa ni wa ushindani na mgumu kutokana na The Cranes nao wana timu nzuri na wamejiandaa kushinda katika mechi hiyo.

Maximo alisema kuwa anawaamini wachezaji wake kuwa wataonyesha kiwango kizuri na kuhakikisha wanashinda katika mchezo huo wa marudiano na kuongeza kuwa bado
wataingia uwanjani wakiwa wanaiheshimu The Cranes kuwa ni moja ya timu nzuri katika ukanda huu.

Alisema kuwa mchezo huo utakuwa ni wa ushindani katika pande zote mbili na amewaeleza vijana wake kuwa waingie uwanjani wakiamini kuwa ndio wanaenda kuanza kazi na kutofikiria mabao 2-0 waliyofunga katika mchezo wa awali.

Alisema kuwa hataki kuona kuwa ari iliyoonyeshwa katika michezo iliyopita inapotea licha ya kuwakosa wachezaji wake muhimu ambao ni Abdi Kassim na Henry Joseph wanaosumbuliwa na majeraha na hivyo kulazimika kutowatumia.

Aliongeza kuwa pengo la majeruhi hao litazibwa na wachezaji wengine walioko katika kikosi hicho ambao wote ubora wao unalingana na kuwataka watanzania wasiwe na hofu juu ya hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, BMT, Iddi Kipingu ambaye aliwakabidhi bendera ya nchi aliwaambia kuwa wanachotakiwa kwenda kukifanya Kampala ni kuleta ushindi.

Kipingu alisema kuwa anaamini maelekezo waliyopewa kabla ya mechi ya kwanza ndio wataendelea kuyafanyia kazi ili kuendeleza furaha walioianza.

``Nendeni mkashinde, mkishinda ndio mtazidi kupendwa na pia kujitengenezea maisha yenu binafsi,`` aliwaasa Kipingu.

Jumla ya wachezaji 22 na viongozi watano wakiongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais, Crescentius Magori wanatarajiwa kuondoka leo kuelekea Kampala kujiandaa na mchezo huo.

  • SOURCE: Nipashe
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.