16 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Watahadharishwa kuzagaa kwa simu feki mitaani
 
2008-05-16 10:14:33
Na Joseph Mwendapole

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewatahadharisha wananchi juu ya kuzagaa kwa simu feki zinazouzwa kwa bei chee madukani na mitaani.

Kufuatia utitiri huo TCRA imewataka wananchi kuacha kukimbilia kununua simu za bei chee kwani nyingi ni bandia na hazidumu hata kwa miezi mitatu.

Tahadhari hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mhandisi wa Mamlaka Bw. Deogratias Moyo, wakati wa maonyesho ya Wiki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) inayomalizika hapa jijini.

Alieleza kushangazwa na ujanja wa kuuza simu feki ambapo simu halisi inauzwa kwa Sh. 400,000 lakini ile ya bandia huuzwa kwa Sh. 45,000.

Alisema kuna simu nyinyi zisizofaa kwa matumizi ambazo zilizoingizwa bila kufuata taratibu na kuuzwa kwa bei nafuu.

Alisema kutokujua kwa baadhi ya watu wamekuwa wakizichangamkia lakini wamekuwa wakikaa nazo kwa muda mfupi.

Bw. Moyo alisema tatizo la bidhaa feki limeenea duniani kote kutokana na kuibuka kwa viwanda vingi vya kutengeneza bidhaa hizo.

Aliwataka wananchi kununua simu katika maduka yanayoaminika ili kuepuka hasara kwani simu hizo hazidumu hata miezi miwili.

Aliwashauri wananchi kuangalia katika mtandao bei za simu halisi kabla ya kununua zile za mitaani ambazo nyingi hudumu muda mfupi.

Aliongeza kuwa wataendelea kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC) ili kuyafungia maduka yote yatakayogundulika kuingiza simu zaba bandia.

Aliongeza kuwa TCRA itajitahidi kuhakikisha kuwa wanaopewa leseni za kuuza vifaa vya kielektronik wanakaguliwa kikamilifu.

Vifaa hivyo ni kama simu, kompyuta, televisheni, kamera na mashine mbalimbali zikiwemo za maofisini, mahospitali na viwandani.

  • SOURCE: Nipashe
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.