27 Sep 2005 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Manispaa ya Kigoma/Ujiji inavunja nyumba za watu waliojenga katika eneo la makaburini
 
2005-09-27 13:59:31
Na Radio One Habari

Manispaa ya Kigoma/Ujiji, mkoani Kigoma inavunja nyumba za watu waliojenga katika eneo la makaburini eneo la Mwanga mjini Kigoma zoezi ambalo limezua ghasia kati ya askari wa manispaa hiyo na wamailiki wa nyumba hizo.

Habari zinasema kuwa zaidi ya nyumba saba zimevunjwa na maaskari wa manispaa hiyo na wao kujikuta wakirushiwa mawe na wamiliki wa nyumba hizo

Wakizungumza na chama cha waandishi wa habari wa mkoa wa Kigoma katika eneo la tukio ,mmoja wa wenye nyumba hizo, Bibi Salma Kalila amedai kuwa zoezi hilo halikufanyika kwa kufuata taratibu.

Bibi Kalila amesema watumisjhi wa manispaa hito walifika eneo hilo siku moja na kuweka alama ya X na siku iliyowafuatia walifika asubuhi na kuanza kuvunja nyumba zao wakati kibali cha kujenga katika eneo hilo na manispaa hiyohiyo.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo ya Kigoma Ujiji , Bwana Laban Tanda amekiri kuvunjwa kwa nyumba hizo na kueleza kuwa ni kweli manispaa haikuwafahamisha wakazi wa eneo hilo la makaburini katika kitongoji cha Mwanga juu ya zoezi hilo kabla ya kuvunjiwa lakini zoezi hilo ni halali.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.