30 Sep 2005 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Vyama vya siasa vimetakiwa kuhubiri mshikamano
 
2005-09-30 17:45:52
Na Radio One Habari

Wito umetolewa kwa vyama vya siasa kuhubiri maneno yatakayoongeza mshikamano na kuepuka vurugu. Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Kazini Pemba, Bwana Ameir Juma Ameir katika kikao cha pamoja na viongozi wa vyama vya siasa kilichotathmini mwenendo wa kampeni za siasa zinavyoendelea Zanzibar.

Amesema utulivu na amani vinaweza kupatikanaa iwapo viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi wao wataonesha ustahimilivu kwa kutotoa kauli za matusi na kashfa.

Kamanda Ameir amesema ni wajibu wa viongozi wa vyama hivyo kusimamiaa usalama wa raia wanapokwenda na kurudi mikutanoni na pia kutoruhusu madereva kwenda mwendo wa kasi na kubeba abiria kupita kiwango.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.