|
Waislamu na Watanzania mjenge umoja
2006-10-24 14:13:38
Na Radio One Habari
Viongozi wa dini ya Kiislamu wamewaomba wafuasi wao na Watanzania kwa jumla kuwa na umoja, kudumisha amani na kuepuka tofauti hasa za dini zinazoweza kuitumbukiza nchi katika migogoro.
Walikuwa wakitoa mawaidha wakati wa swala za Iddi el Fitr katika sherehe za kuadhimisha mwisho wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambazo kitaifa zinafanyika Arusha.
Kwenye swala iliyofanyika Uwanja wa Michezo wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha Mufti wa Tanzania, Mufti wa Tanzania Sheikh Mkuu Issa Bin Shaaban Simba amewataka Waislamu na Watanzania kwa jumla kujenga umoja.
Amesema ni wajibu wa kila mwislamu, awe kiongozi au mfuasi na watu wote kwa jumla nchini, kujenga umoja na kwamba wakati umekwisha wa watu kugombana, kufarakana, kuwa na fitna na kutengana.
Jioni hii Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuhutubia Baraza la IDD ambalo litafanyika kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, cha AICC mjini Arusha.
|