|
Nitashirikiana na serikali kuhudumia jamii-Mch. Lupaa
2006-10-25 14:52:07
Na Radio One Habari
Serikali mkoani Singida imesema inaheshimu na kuthamini mchango wa huduma mbalimbali za kijamii unaotolewa kwa wananchi na mashirika na taasisi za madhehebu ya dini nchini.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Bi. Florence Horombe amesema hayo kwenye ibada ya kumuweka wakfu askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Rift Valley-Manyoni Mchungaji John Lupaa.
Amezitaja baadhi ya huduma hizo kuwa ni pamoja na kuanzisha shule ya Sekondari na vyuo, Hospitali, visima vya maji, kulea watoto waishio katika mazingira magumu na walioachwa yatima na wazazi au walezi wao kutokana na ugonjwa wa UKIMWI.
Bi. Horombe amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa mashirika na taasisi hizo ili ziweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo ya kuwahudumia wananchi kiroho na kimwili.
Kwa upande wake askofu mpya wa dayosisi ya Rift valley mchungaji John Lupaa ameahidi kushirikiana na vingozi wa serikali katika kuihudumia jamii.
|