|
Waziri Mkuu wa Msumbiji kufanya ziara nchini
2006-10-25 14:54:25
Na Radio One Habari
Ujumbe maafisa saba ukiongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Jenerali Mastaafu Tobias Dai uko nchini kwa ziara rasmi ya siku tano.
Ziara ya ujumbe huo ina lengo la kudumisha na kuendeleza uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Msumbiji na baina ya majeshi ya nchi hizi mbili.
Ukiwa nchini ujumbe huo utatembelea maeneo mbalimbali katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Arusha .
Aidha ujumbe huo utakuwa na mazungumzo rasmi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Prof. Juma Kapuya yanayolenga kuboresha uhusiano baina ya majeshi ya Tanzania na Msumbiji.
Jenerali mstaafu Dai na ujumbe wake anatarajiwa kuondoka nchini Jumapili ijayo kurejea Msumbiji.
|