|
Waislamu wametakiwa kudumisha mshikamano
2006-10-25 14:55:06
Na Radio One Habari
Waislamu nchini wameshauriwa kuendeleza mshikamano na uadilifu kama walivyofanya wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh wa Msikiti wa Wilaya ya Songea Mjini, Ustaadh Shaibu Mohamed ametoa changamoto hiyo katika salamu zake za sikukuu ya Eid-El-Fitr.
Ustaadh Mohamed amesema ni vyema waislamu wakadumisha mshikamano na umoja wa kijamii baina yao na hata waumini wa dini zingine.
Amewataka Waislamu kusherehekea Eid kwa furaha na kuwasaidia wote wenye shida na baada ya hapo waendelee kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
|