|
Tuweka kituo maalum kitakachotuwezesha kupata habari za biashara duniani
2006-10-25 14:55:36
Na Radio One Habari
Wafanyabisahara wa Jiji la Tanga wameliomba Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa –UNIDO- kusaidia kuweka kituo maalum kitakachowawezesha kupata habari za biashara duniani.
Ushauri huo umetolewa na wafanyabiashara wadogo wa jiji hilo kwenye warsha ya siku moja iliyohusu elimu juu ya wafanyabiashara kutambua umuhimu wa mawasiliano ya biashara na utandawazi.
Wafanyabiashara hao kutoka sekta ya biashara ndogo ndogo na za kati, wamesema ili kushindanisha biashara kwa ubora wa bidhaa, wanapaswa kujua namna ya kuendesha biashara katika utandawazi kwa kupata habari za biashara zinazofanyika ndani na nje ya nchi.
Wamesema ili kukabiliana na ushindani wa biashara katika ushirikiano wa Afrika Mashariki na kunufaika nao, hawana budi kuwa na kituo maalumu cha kuwawezesha kufahamu yanayofanyika nchi jirani.
Awali, mkufunzi mkuu wa mafunzo hayo ambaye ni Mwakilishi wa UNIDO katika Afrika Mashariki, Bw. Vijit Ratnarajan alisema mkakati wa shirika hilo ni kukuza na kuimarisha vituo vya upashanaji habari za biashara kati ya wafanyabiashara wadogo na wa kati.
|