13 Nov 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Englishnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakazi wa Kigamboni kuopata kivuko kipya baada ya mwaka mmoja
 
2006-11-13 16:18:57
By Radio One Habari

Serikali imesema kivuko kipya kwa ajili ya kutoa huduma ya kuvusha wananchi katika eneo la Feri Kigamboni jijini Dar es Salaam kitapatikana baada ya mwaka mmoja.

Akijibu swali Bungeni Naibu Waziri wa Miundombinu DR. Makongoro Mahanga amesema kampuni itakayoleta kivuko hicho tayari imekwishatia saini makubaliano hayo.

Pia amesema kwa sasa wizara yake inakifanyia ukarabati kivuko cha Mv. Kigamboni ili kiweze kutoa huduma baada ya kupata kibali kutoka Benki ya Dunia.

Naye Naibu Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji Dr. Batilda Burian amesema kiwango cha uandikishaji wanafunzi katika shule za msingi kimepanda kutoka asilimia 77.6 mwaka 2000 hadi asilimia 109.9 mwaka 2005 ambayo ni zaidi ya kiwango kilichowekwa cha malengo ya milenia.

Akijibu swali Bungeni pia amesema kwa kila vizazi hai elfu moja idadi ya vifo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano imepungua kutoka vifo 147 mwaka 1999 hadi vifo 112 mwaka 2004 wakati vifo vya watoto chini ya umri wa mwaka mmoja vimepungua kutoka 99 mwaka 1999 hadi vifo 68 mwaka 2004.

  • SOURCE: Radio One
 
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Recent features
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.