27 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mkoa wa Kilimanjaro kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 46
 
2006-12-27 18:32:04
Na Radio One Habari

Mkoa wa Kilimanjaro umetenga zaidi ya shilingi Bilioni 46 na Milioni 400 kwa ajili ya matumizi mbali mbali na shughuli za maendeleo katika bajeti yake ya mwaka 2006/07.

Akiwasilisha taarifa ya bajeti katika kikao cha kamati ya ushauri na maendeleo ya mkoa Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa huo Bwana Reginald Kombania amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya shughuli mbali mbali za maendeleo ya mkoa na wilaya zote.

Amesema zaidi ya shilingi Bilioni Tatu na Milioni 800 ni kwa ajili ya mkoa na zaidi ya shilingi Bilioni 42 na Milioni 700 ni kwa ajili ya halmashauri za wilaya.

Bwana Kombania amesema kwa upande wa miradi ya maendeleo mkoa huo umepata zaidi ya shilingi Bilioni Moja na Milioni 400 zilizoidhinishwa na bunge, ambapo miradi inayogharimiwa na mkoa itatumia zaidi ya shilingi Milioni 539 na Laki tisa na wilaya zaidi ya shilingi Mililioni 215.

Amefafanua kuwa hatua iliyofikiwa katika kuhakikisha miradi hiyo zaidi ya 33 inatekelezwa ni ukamilishaji wa zabuni za kutekeleza miradi hiyo.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.