31 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wachimbaji zaidi ya 600 kuondolewa Buhemba
 
2006-12-31 15:48:58
Na Radio One Habari

Wilaya ya Musoma mkoani Mara imetangaza operesheni maalum ya kuwaondoa wachimbaji zaidi ya 600 wa dhahabu waliovamia eneo la mgodi wa Buhemba katika kijiji cha Magunga kinyume cha utaratibu.

Mkuu wa wilaya ya Musoma Bw. Saveli Maketa ametangaza operesheni hiyo alipokuwa akizungumza na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.

Amesema serikali itaanza kuwaondoa wachimbaji hao mwezi ujao ili kuruhusu kampuni ya Landgold inayochimba dhahabu katika mgodi wa Buhemba kuendelea na shughuli zake baada ya kampuni hiyo kusimamisha uzalishaji mwezi uliopita kutokana na kupungua kwa dhahabu katika eneo la zamani.

Habari zinasema msimamo huo wa serikali wa kutaka kuwaondoa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu katika eneo la mgodi huo wa Buhemba unatofautiana na msimamo wa Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Mhe. Nimrod Mkono, ambaye amekuwa akiitaka serikali iweke utaratibu wa kuwatengea wachimbaji hao maeneo mengine ya kuchimba dhahabu kwa vibali maalum.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.