31 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Matatizo ya Uzazi yauwa wanawake 16 Iramba
 
2006-12-31 15:49:37
Na Radio One Habari

Wanawake 16 wamefariki dunia katika wilaya ya Iramba mkoani Simgida kutokana na matatizo mbalimbali ya uzazi kati ya Januari hadi Oktoba mwaka huu.

Taarifa ya idara ya afya ya wilaya hiyo imesema hayo wakati wa majumuisho ya mafunzo ya uzazi salama kwa wakazi wa vijiji vya Kaselya, Mgungira na Mwanduigembe yaliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la \’Utu mwanamke\’ lenye makazi yake jijini
Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mwaka huu vifo vya wanawake kutokana na matatizo ya uzazi vimeongezeka zaidi ikilinganishwa na vifo 12 vilivyotokea katika kipindi cha mwaka jana.

Imesema vifo hivyo huchangiwa na sababu mbalimbali, zikiwemo kifafa cha mimba na elimu duni ya uzazi salama.

Akitoa taarifa hiyo mjini Kiomboi, Mratibu wa mafunzo hayo kutoka shirika hilo la ’Utu mwanamke, Bibi Catherine Kamungumia ameishauri wilaya ya Iramba ivisaidie vijiji hivyo vya Kaselya, Mgunira na Mwanduigembe ili viweze kuanzisha mfuko maalum utakaowezesha kuwahudumia wanawake wajawazito wasio na uwezo.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.