31 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mvua kubwa yaharibu mfumo wa maji Arusha
 
2006-12-31 15:50:27
Na Radio One Habari

Mvua kubwa zinazoambatana na upepo mkali ambazo zimenyesha siku tatu mfululizo katika safu ya mlima Meru katika wilaya ya Arusha imesababisha kuharibika kwa mifumo ya maji katika baadhi ya maeneo ya manispaa ya Arusha.

Kwa mujibu wa Idara ya habari- Maelezo, mkoani Arusha, mvua hizo pia zimesababisha baadhi ya maeneo kama vile Serengeti, Engira, Njiro, Kijenge na mitaa ya maeneo ya Ikulu kukosa maji tangu tarehe 29 mwezi huu kutokana na mabomba kuziba baada ya kujaa mchanga na takataka nyingine ngumu.

Maeneo mengine yaliyokumbwa na athari za mvua hizo ni pamoja na maeneo ya kati ya mji wa Arusha katika soko kuu la Arusha, Sokoni One na maeneo ya Daraja Mbili.

Baadhi ya wananchi waliohijiwa na Maelezo katika mitaa ya Engira, Serengeti ba Ikulu, wamesema wameanza kukosa maji kuanzia tarehe 28 mwezi huu na wamegundua kuwa baadhi ya mabomba yameziba kutokana na kujaa mchanga.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.