31 Dec 2006 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Waislam wametakiwa kudumisha umoja na mshikamano
 
2006-12-31 15:52:46
Na Radio One Habari

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amewasihi Waislamu nchini kuwa na mshikamano na kudumisha umoja na amani miongoni mwao na waumini wa dini nyingine ili kudumisha amani iliyopo nchini.

Akihutubia Baraza la Idd katika msikiti wa Manyema jijini Dar es Salaam leo, Alhaji Mwinyi amesema Muislamu ni yule ambaye wenzake wanasalimika na shari ya ulimi na mikono yake,

Amesema Tanzania ni kisiwa cha amani ambacho kimewafanya hata watu kutoka nchi jirani zenye matatizo kukimbilia, hivyo hapana budi kuilinda amani na kusisitiza Waislamu wasikubali mtu au kikundi cha watu kwa kutumia jina la Uislamu kuvuruga amani.

Aidha, Rais huyo mstaafu, ameonya juu ya ugonjwa wa Ukimwi na kuitaka jamii ichukue kila tahadhari kujiepusha na janga hili, ikiwa pamoja na kuwa waaminifu katika ndoa na kwa wale wasiokuwa na ndoa watafute ndoa salama.

Awali, Naibu Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, pamoja na mambo mengine, aliwakumbusha Waislamu kutekeleza wajibu wao, wakiwa sehemu ya jamii, kwa kuwasaidia yatima, wajane, watoto wa mitaani na wazee.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.