04 Jan 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kina cha maji katika Bwawa la Mtera chaongezeka
 
2007-01-04 17:33:24
Na Radio One Habari

Kufuatia mvua zinazonyesha katika mikoa ya Iringa na Mbeya kina cha maji katika Bwawa la Mtera kinaendelea kuongezeka ambapo sasa kimefikia mita 692.45 kutoka usawa wa bahari.

Afisa wa maji bonde la Rufiji Bwana Willy Mwaluvanda amesema wastani wa maji yanayoingia katika bwawa hilo kutoka mito mbalimbali kwa sasa ni mita za ujazo 671 kwa sekunde.

Bwana Mwaluvanda amesema mpaka sasa bwawa hilo bado halijaanza kuzalisha umeme tangu lifungwe mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kina cha maji katika bwawa hilo kupungua zaidi.

Amesema kuongezeka kwa kina cha maji katika bwawa hilo ni matokeo ya juhudi za uhifadhi wa mazingira katika bonde la Usangu ambazo pia zimesaidia kupunguza siku za kukauka kwa mto Ruaha Mkuu.

Kuhusu bwawa la Kidatu, Bwana Mwaluvanda amesema kina kimefikia mita 449.12 na kwamba maji yanayoingia kwenye bwawa hilo ni mengi kutosheleza uzalishaji wa umeme ingawa wakati mwingine inalazimika kuyamwaga.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.