04 Jan 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Juma Akukweti afariki dunia
 
2007-01-04 17:34:29
Na Radio One Habari

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Juma Jamaldin Akukweti amefariki dunia katika hospitali moja mjini Johannesburg huko Afrika ya Kusini.

Mheshimiwa Akukweti alipelekwa Afrika ya Kusini kwa matibabu zaidi kutokana na majeraha ya moto kufuatia ajali ya ndege iliyotokea Mbeya tarehe 16 mwezi uliopita.

Akitoa taarifa ya kifo chake kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete Katibu Mkuu wa Ikulu Bibi Rose Lugembe amesema taratibu zinafanywa kurejesha mwili wa marehemu hapa nchini kwa mazishi.

Marehemu Akukweti alikuwa miongoni mwa watu sita waliokuwemo katika ndege hiyo na kufanya idadi ya watu waliokufa kutokana na ajali hiyo kufikia wanne.

Wengine ni mpiga picha wa Idara ya Habari Maelezo Bibi Theresia Nyantori aliyekufa papo hapo, Mratibu wa Programu ya Uendelezaji Mifumo ya Masoko ya Mazao ya Kilimo Bwana Nathaniel Katinila na Afisa Habari wa Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bwana George Bendera.

Wengine waliokuwa kwenye ajali hiyo ni rubani wa ndege hiyo Martin Sumari na Nisetas Kanje, ambaye ni Msaidizi wa Waziri Akukweti ambaye bado anatibiwa katika Hospitali ya taifa ya Muhimbili.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2005 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.