22 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mkoa wa Mbeya umejenga shule mpya 60 za sekondari
 
2007-04-22 15:24:42
Na Radio One Habari

Mkoa wa Mbeya mwaka huu umejenga zaidi ya shule mpya 60 za sekondari ambazo zimewezesha wanafunzi elfu-29 kati ya 38-elfu na 600 waliofaulu mtihani wa darasa la saba kuanza kidato cha kwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. John Mwakipesile amesema idadi ya wanafunzi waliojiunga na sekondari hizo ni sawa na asilimia 82 ambapo wanafunzi wengine 9,600, sawa na asilimia 18 hawajajiunga na shule za sekondari za serikali na badala yake wanakwenda shule za watu binafsi.

Akizungumza baada ya kutembelea shule ya sekondari ya Mlima Mbeya na kuzungumza na wanafunzi, wafanyakazi na viongozi wa shule hiyo Bw. Mwakipesile amesema mkoa wake unaendelea kufuatilia ili kujua ni wanafunzi wangapi waliobaki.

Amesema idadi ya shule za sekondari zilizojengwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na ile ya mwaka jana ambapo zilijengwa shule 40 na kuchukua wanafunzi 20-elfu tu na wengine 8,000 kukosa nafasi.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.