22 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

UN-HABITAT kusaidia vijana Afrika Mashariki
 
2007-04-22 15:25:14
Na Radio One Habari

Shirika la makazi la umoja wa Mataifa UN-HABITAT limeandaa mpango wa kuwasidia vijana kukabiliana na changamoto mbalimbali katika nchi za Afrika mashariki na kati ikiwemo Tanzania.

Mwakilishi wa Tanzania aliyehudhuria mkutano wa Baraza Kuu la shirikisho hilo uliomalizika jana mjini Nairobi, Kenya Bw. Philemon Mutashubirwa amesema hatua za awali za utekelezaji wa mpango huo zinatarajiwa kuanza katikati ya mwaka huu.

Bw. Mutashubirwa amesema hatua hizo ni pamoja na kujenga vituo vya vijana katika maeneo mbalimbali na kwamba kituo cha kwanza kitajengwa jijini Dar es Salaam.

Amesema shirika hilo limefikia hatua hiyo kutokana na kutambua umuhimu wa vijana katika utatuzi wa matatizo mbalimbali na kwamba vijana wanaweza kutoa mchango mkubwa katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo la makazi.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.