|
Maiti wawili wa ajali ya Buffalo bado kutambuliwa
2007-04-22 15:25:50
Na Radio One Habari
Maiti wawili ambao ni miongoni mwa watu 22 waliofariki dunia katika ajali ya basi la Buffalo Mkoani Kilimanjaro baada ya kugongana na lori la mafuta Jumapili iliyopita bado hawajambuliwa.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Bw. Lucas Ng`hoboko amesema maiti hao ni mwanamke na mwanamme ambao wapo katika hospitali ya rufaa ya KCMC na Mawenzi mjini Moshi.
Amesema, maiti ya mtu mwingine wa 20 imetambuliwa kwa jina la Leonard Saria wa Kibosho Moshi ambaye alikuwa dereva wa basi dogo linalotoa huduma za usafiri kati ya Kiborloni na mjini Moshi.
Kamanda Ng`hoboko amesema majeruhi wanne kati ya 18 waliokuwa wamelazwa bado wapo hospitali ya KCMC, akiwemo dereva wa basi la Buffalo Emmanuel Kessy ambaye yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Wengine ni Peter Msafiri wa Kibosho Moshi vijijini, Samwel Anaeli wa Arusha na Zaituni Lihata wa Mbagala Dar es Salaam.
|