|
Vijiji kupatiwa mashine za kufyatua matofali
2007-04-22 15:26:25
Na Radio One Habari
Baadhi ya halmashauri za mkoa wa Shinyanga zimeanza kusambaza mashine za kufyatulia matofali zenye gharama nafuu kwa lengo la kuwawezesha wananchi wa vijijini kujenga nyumba bora na kuondokana na nyumba duni.
Mashine hizo zimetengenezwa maalum kwa ajili ya kufyatua matofali ya udongo, saruji na ya kuchoma.
Wakitoa taarifa hizo kwa nyakati tofauti wakurugenzi watendaji wa halmashauri za Meatu, Bariadi na Kahama wamesema zoezi la kugawa mashine hizo limeanza katika kata za halmashauri.
Mmoja wa Wakurugenzi hao , Bw. Paul Chiwele wa halmashauri ya Meatu amesema mashine hizo tayari zimesambazwa katika kata za tarafa tatu ambako wananchi watajifunza jinsi ya kuzitumia na kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zenye gharama nafuu.
|