|
Waziri wa Kilimo wa Indonesia kuwasili kesho
2007-04-22 15:27:25
Na Radio One Habari
Waziri wa Kilimo wa Indoneshia, Dakta Anton Apriyantono anawasili nchini kesho kwa ziara ya siku tatu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili katika kuendeleza sekta ya kilimo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika katika ziara hiyo Bw. Apriyantono ataongoza ujumbe wa watu 15, wakiwemo wafanya biashara.
Akiwa nchini atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Kilimo, Chakula na ushirika, Mhe. Stephen Wasira na wadau wengine kuhusu nyanja za ushirikiano katika sekta ya kilimo.
Mazungumzo hayo yatafuatiwa na mkutano utakaojumuisha wafanya biashara wa Tanzania na Indonesia.
Aidha ujumbe huo wa Indonesia utatembelea kituo cha mafunzo ya Wakulima cha Mkindo mkoani Morogoro.
|