23 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Waalimu wa MEMKWA Musoma walalamikia mishahara
 
2007-04-23 18:52:16
Na Radio One Habari

Waalimu binafsi wanaofundisha madarasa ya Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa –MEMKWA- katika Manispaa ya Musoma Mkoani Mara wameilalamikia serikali kwa kuwacheleweshea mishahara yao kwa muda wa miezi minne sasa.

Akizungumza na PST Mjini Musoma, mmoja wa waalimu hao kwa niaba ya wenzake amesema mishahara hiyo haijalipwa tangu Januari mwaka huu na kwamba kila mmoja anadai Shilingi Elfu-80 kwa miezi yote minne.

Mwalimu huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kila wanapofuatilia fedha hizo katika ofisi ya Ofisa elimu wa Manispaa ya Moshi wamekuwa wakiambiwa kuwa fedha zao hazijapelekwa huko kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.