23 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Hakuna wakimbizi wa ziada wa Burundi wanaoishi Tanzania
 
2007-04-23 18:54:29
Na Radio One Habari

Serikali ya Marekani imesema hakuna wakimbizi wa ziada kutoka Burundi wanaoishi katika makambi mbalimbali nchini Tanzania watakaochukuliwa kwenda kupewa makazi mapya nchini Marekani.

Afisa wa Uchumi na Siasa wa Ubalozi wa Marekani Maureen Latour amesema zaidi ya wale ambao wameshatambuliwa na kufanyiwa taratibu za kwenda kuishi Marekani hadi sasa hakuna wengine watakaokwenda huko.

Amesema hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa wakimbizi wa Burundi katika kambi ya Muyowosi, Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma waliotaka kupatiwa nafasi ya kwenda kuishi nchini Marekani.

Alikuwa akizungumza wakati wa msafara wa ziara ya Balozi wa Hispania nchini Burundi na Tanzania, Bwana German Zuritta na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzani, Bwana Wolfgang Ringe Mkoani Kigoma.

Walikwenda kujionea utekelezaji wa zoezi la kuwarudisha wakimmbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Burundi wanaoishi mkoani humo.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.