29 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kuna ukosefu wa demokrasia ya kutosha Jumuiya ya Afrika Mashariki
 
2007-04-29 15:19:06
Na Radio One Habari

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Juma Mwapachu amesema kuna ukosefu wa demokrasia ya kutosha katika kuwashirikisha wananchi wa nchi wanachama kuhusu maamuzi yanayofanywa na viongozi ya mipango na sera mbalimbali.

Balozi Mwapachu amesema hayo wakati wa mkutano wa vyombo vya habari vya Afrika Mashariki ulioandaliwa kwa pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki jijini Nairobi, nchini Kenya.

Amesema kasoro hiyo inaweza kurekebishwa iwapo vyombo vya habari vitashirikishwa ipasavyo katika kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu sera na miradi ya jumuiya hiyo.

Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri wa Afrika Mashariki wa Kenya, Mhe. Bonny Kihwale amesema tangu kuanzishwa upya kwa jumuiya hiyo kumekuwa na mafanikio na maendeleo makubwa na kwamba upo mkakati wa miaka mitano wa kuitangaza jumuiya kwa kushirikisha sekta binafsi, umma na vyombo vya habari.

Akiwasilisha mada kuhusu jukumu la vyombo vya habari vya Afrika Mashariki katika mchakato wa kuanzishwa kwa shirikisho la Afrika Mashariki na kuvutia utalii na biashara, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Bwana Reginald Mengi amevitaka vyombo vya habari kuacha ukasuku wa kuchapisha bila kuchuja habari potofu zinazoenezwa na vyombo vya habari vya magharibi.

Badala yake amevitaka vyombo hivyo kulinda taswira njema ya Afrika Mashariki kwa kukosoa kila upotoshaji huo wa habari unapofanyika.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.