|
Kigoma waanza kukusanya damu salama
2007-04-29 15:19:51
Na Radio One Habari
Halmashauri ya wilaya ya Kigoma kwa kushirikiana na chama cha msalaba mwekundu mkoani humo imeanzisha utaratibu wa kukusanya damu salama kutoka kwa wananchi ili kusaidia wagonjwa wenye upungufu wa damu wanaofikishwa katika hospitali ya mkoa wa Kigoma ya Maweni.
Mganga mkuu wa wilaya ya Kigoma Dk. Dismas Vyagusa amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Kazuramimba.
Amesema kutokana na mahitaji ya damu katika benki ya damu ya hospitali hiyo wananchi wanapaswa kuendelea kuchangia ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye upungufu wa damu.
Naye mratibu wa Damu salama kutoka chama cha msalaba mwekundu Dk. Anna Kichambati amesema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita uniti 3150 za damu zilipatikana.
|