29 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kuhama kwa wazazi Kigoma kunachochea utoro
 
2007-04-29 15:22:33
Na Radio One Habari

Uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa wilayani Kigoma unasababisha kukithiri kwa utoro wa wanafunzi wa shule za msingi kutokana na wazazi kuishi kwa kuhamahama na kuwatumia watoto wao kutafuta kuni.

Afisa elimu wa wilaya ya Kigoma Bwana Maya Mlangi amesema hayo wakati akifungua semina kwa walimu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo.

Semina hiyo ililenga kuweka mkakati wa kuwashirikisha wanafunzi katika hifadhi ya mazingira ili wakue wakielewa umuhimu wa kuhifadhi mazingira.

Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo wamesema juhudi za kuhifadhi mazingira sasa zielekezwe kwa watoto wadogo ili kuwajengea msingi wa kuthamini mazingira.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.