29 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Waandishi lindeni maslahi ya taifa
 
2007-04-29 15:24:09
Na Radio One Habari

Waandishi wa habari wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi na maadili ya taaluma sanjari na kulinda maslahi ya taifa kwa mataifa mengine.

Wito umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Morogoro Bw, Saidi Mwambungu wakati akifungua mkutano wa siku moja wa wadau wa habari kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Lindi na Morogoro.

Amesema vyombo vya habari vina wajibu wa kuandika na kukosoa yanayostahili kukosolewa kwa maslahi ya wananachi na taifa kwa ujumla lakini viepuke habari zisizofanyiwa kazi kwa kina ambazo mara kadhaa zimekuwa zikizua migogoro ama kukidhalilisha chombo husika.

Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la habari Tanzania -MCT- na umoja wa vyama vya waandishi wa habari vya mikoa –UTPC- kwa lengo la kukusanya maoni ya wadau juu ya mapendekezo kuhusu muswada wa sheria ya uhuru na haki ya kupata habari ya mwaka 2007.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.