29 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Benki ya Dunia yaipatia Zanzibar dola za Marekani milioni 42
 
2007-04-29 15:25:29
Na Radio One Habari

Benki ya Dunia imeidhinisha dola za Marekani milioni 42 kusaidia juhudi za kuinua sekta ya elimu visiwani Zanzibar.

Kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya dola za Marekani milioni 48 zinazotarajiwa kuinua elimu visiwani katika kipindi cha miaka sita ijayo.

Taarifa ya Benki hiyo imesema mradi huo unalenga kuimarisha elimu ya sekondari na kuwawezesha wanafunzi kupata matokeo mazuri katika mitihani yao.

Hatua hizo zinajumuisha ujenzi wa madarasa, maabara, na kuinua mafunzo kwa walimu ikiwemo viwango vya ufundishaji masomo ya sayansi na hisabati na ununuzi wa vitabu.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.