30 Apr 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Sheria itakayoongoza mifuko ya hifadhi ya jamii kuundwa
 
2007-04-30 15:47:56
Na Radio One Habari

Serikali iko mbioni kuandaa rasimu ya sheria itakayoongoza utendaji wa shughuli za mifuko ya hifadhi ya jamii hapa nchini ili kuondoa kasoro za utendaji zilizopo hivi sasa.

Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, amesema sheria hiyo itasaidia pia utekelezaji wa sera ya taifa ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2003 inayopendekeza kuundwa kwa chombo kimoja kitakachosimamia mifuko yote.

Bwana Luhanjo alikuwa akizungumza wakati wa warsha ya makatibu wakuu wa wizara za serikali kuhusu uboreshaji wa mifuko hiyo hapa nchini.

Nao baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wamesema iwapo sheria hiyo itaundwa itasaidia kupunguza kasoro zilizopo ndani ya mifuko ya hifadhi ya jamii.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.