24 Aug 2007 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakulima wa tumbaku Manyoni wajipatia zaidi ya Shilingi Milioni 755
 
2007-08-24 18:08:51
Na Radio One Habari

Wakulima wa tumbaku wilayani Manyoni Mkoani Singida wamejipatia zaidi ya Shilingi Milioni 755 na Laki-8 katika msimu wa 2006/2007 kutoka na mauzo ya tani 714.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Bi. Agnes Kitundu, alipozungumza na PST kuhusu maendeleo ya sekta ya kilimo wilayani humo.

Amesema karanga ni zao la pili ambalo liliwaingizia wakulima wa wilaya hiyo Shilingi Milioni 450 kutokana na mauzo ya tani 1,500, wakati Shilingi Milioni 281 na Laki-6 zilipatikana kutokana na mauzo ya tani 2,816 za alizeti.

Mkurugenzi huyo amesema licha ya mazao hayo ardhi nzuri ya wilaya hiyo inafaa kwa kilimo cha mazao mengine kama vile pamba, dengu na ufuta.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.