17 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Serikali kuanzisha maghala ya kuhifadhia mazao nchini kote
 
2008-03-17 17:52:03
Na Radio One Habari

Serikali imepanga kuanzisha maghala ya kuhifadhi mazao kote nchini ili yasaidie kuongeza bei ya mazao na kuharakisha maendeleo ya wakulima na ukuaji uchumi kwa jumla.

Aidha katika kuimarisha sekta ya kilimo serikali imeanza kuzungumza na makampuni ya nje yatakayoweza kujenga viwanda vya kutengeneza zana za kilimo yakiwemo matrekta madogo na makubwa na pembejeo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Peter Msolla wakati akizungumza na wakulima wa kijiji cha Ruaha Mbuyuni katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Amesema chini ya mkakati huo serikali itapenda kuona wakulima wengi wanatumia zana za kisasa ili kuacha jembe la mkono na kuzalisha chakula cha kutosha kwa matumizi ya ndani na kupata ziada ya kuuza nje ya nchi.

Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa minne pamoja na Mbeya, Rukwa na Ruvuma ambayo miaka ya nyuma ilikuwa maarufu kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali ya chakula na hasa mahindi.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.