|
Majambazi wanne wafikishwa mahakamani Chato
2008-03-23 15:19:05
Na Radio One Habari
Polisi Wilayani Chato Mkoani Kagera imewafikisha Mahakamani watuhumiwa wanne wa ujambazi wanaotumia silaha wanaojihusiha na uwindaji haramu katika hifadhi ya taifa Kisiwa cha Rubondo.
Hiyo imetokana na baadhi ya wananchi kubaini nyama wanazouziwa mitaani ni za wanyamapori.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Bwana Abdallah Msika amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Mateso Mathias, Thomas Peter, Baraza Kaza na George Mzilaeli.
Kamanda Msika amesema watu hao wamekutwa wakimiliki bunduki aina ya Shotgun, risasi tatu, nyama ya Kiboko na Nzohe ikiuzwa mitaani wakati watu hao hawana bila kibali cha uwindaji.
Amesema baada ya uchunguzi wa polisi umebaini watuhumiwa hao ni majambazi sugu ambao wamekuwa wakitafutwa kwa tuhuma ya mauaji, ujambazi wa kuteka magari, unyang`anyi wa kutumia silaha na uwindaji haramu katika maeneo ya mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Kagera.
|