23 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Mradi wa maji Lindi wahitaji zaidi ya milioni 500
 
2008-03-23 15:20:01
Na Radio One Habari

Mradi mkubwa wa maji wa Nyangao-Mtama, mkoani Lindi, ambao mtandao wake wa mabomba una jumla ya kilomita 44, unahitaji shilingi zaidi ya milioni 500 ili uweze kukamilika.

Mradi huo ambao ni wa maporomoko, chanzo chake kinatokana na mto Nyangao katika eneo la Chiuwe wilaya ya Lindi vijijini na utakapokamilika, utatoa huduma kwa zaidi ya wananchi 23,722 wa vijiji 7 vya Mtakuja, Cheleweni, Ng’au, Nang’aka, Majengo, Masasi, Makonde, Mihogoni na Mkwajuni.

Taarifa ya ujenzi wa mradi huo iliyotolewa na Mhandisi wa maji wa halmashauri ya wilaya ya Lindi, Bwana Mbaraka Kilangai imeeleza kuwa mpaka sasa ujenzi wa mradi huo ambao ulianza mwaka 2004/2005, umegharimu shilingi zaidi ya milioni-184.

Kwa mjibu wa Mhandisi huyo, kazi zilizofanyika mpaka sasa ni pamoja na ujenzi wa kitekeo cha maji chenye ujazo wa mita za ujazo 18, ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa mita za ujazo 270 na ununuzi wa mabomba 1,625 yenye kipenyo cha nchi 6.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.