23 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Kampuni ya mbolea India kujenga kiwanda Mtwara
 
2008-03-23 15:21:09
Na Radio One Habari

Kampuni ya kutengeneza mbolea ya Deepak iliyoko Mumbai nchini India imeeleza nia yake ya kutaka kujenga kiwanda cha mbolea mkoani Mtwara kitakachotumia gesi kama mali ghafi katika kuzalisha bidhaa hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bwana Sailesh Mehta amemweleza hayo Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein ambaye yuko katika ziara ya kikazi nchini India.

Amesema ameshakutana na kujadiliana na maofisa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wale wa Wizara ya Nishati na Madini juu ya suala hilo na kilichobaki sasa ni utekelezaji wa taratibu zitakazoharakisha uanzishwaji wa mradi huo.

Bwana Mehta amebainisha kuwa mpango wa kuitumia gesi hiyo kwa kutengeneza mbolea itakuwa ni njia nzuri ya kuendeleza uchumi wa Tanzania na kwamba mradi huo utahusisha mtaji wa dola za kimarekani milioni-505 na utatoa ajira kwa watu 275 watakaoendesha mitambo ya kiwanda.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Makamu wa Rais, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dk. Mary Nagu amesema serikali inakaribisha mradi huo, kutokana na ukweli kwamba kiwanda cha mbolea kitatoa msingi imara katika kukuza kilimo nchini Tanzania.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.