24 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Miradi ya maji yagharimu zaidi ya shilingi milioni 32 mikoa ya Singida, Shinyanga na Tabora
 
2008-03-24 16:56:46
Na Radio One Habari

Zaidi ya shilingi milioni 32-na-laki-7 zimetumika kwa ajili ya miradi ya maji katika mikoa ya Singida, Shinyanga na Tabora.

Fedha hizo zimetumika kupima mabwawa manne mkoani Shinyanga na kufanya utafiti wa upatikanaji wa maji ardhini katika vijiji 31 vya mikoa ya Tabora na Singida.

Afisa wa Bonde la Kati lenye makao yake makuu mjini Singida Bwana Mtoi Kanyawanah ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa yake ya utendaji kazi kwenye kikao cha bodi.

Amefafanua kuwa baada ya utafiti huo maandalizi yote yamekwisha kamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa utekelezaji wa miradi hiyo wakati wowote.

Amesema lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi katika maeneo hayo wanapata huduma ya maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya majumbani na mifugo yao.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.