24 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wananchi wa Nakatunguru Ukerewe wahoji ushuru wa soko
 
2008-03-24 16:58:45
Na Radio One Habari

Wananchi wa Kata ya Nakatunguru Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza wamehoji uhalali wa halmashauri yao kutoza ushuru katika soko dogo lililomo kwenye Kata hiyo bila kutenga sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya maendeleo ya kata.

Walitoa kero hiyo kwa Mbunge wa jimbo la Ukerewe Mheshimiwa Getrude Mongella wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mtoni katika kata hiyo.

Walidai kuwa kwa muda mrefu sasa halmashauri hiyo imekuwa ikikusanya ushuru katika soko hilo maarufu kama ``Soko Mjinga`` pasipo kutenga sehemu ya fedha kusaidiai maendeleo ya kata hiyo.

Kwa upande wake Mheshimiwa Mongella amesema kimsingi halmashauri inapaswa kutenga fedha kutokana na makusanyo yake ya ndani kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya kila kata.

Amesema kushindwa kutenga fedha kusaidia maendeleo katika kata ni udhaifu uliopo katika uongozi wa halmashauri.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.