|
Mpango wa kupambana na malaria wazinduliwa Ruvuma
2008-03-24 17:00:45
Na Radio One Habari
Wadau wa sekta ya afya Mkoani Ruvuma wametakiwa kuelekeza zaidi nguvu zao katika kupambana na ugonjwa wa malaria ambao kwa sasa unachangia vifo vingi vya watoto na wajawazito mkoani humo.
Changamoto hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bwana Claudio Bitegeko alipozindua mpango wa Milenia wa kupambano na ugonjwa wa Malaria mkoani humo unaotekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya Ores Tanzania na COTN.
Amesema elimu zaidi inahitajika kwa wananchi ili kuweza kupambana na Malaria unasababisha vifo vingi vya watoto na wajawazito.
Akisoma risala ya mashirika hayo mawili Mratibu wa mradi huo Bwana Max Mahudi alisema shirika la ORES Tanzania mbali ya kuendesha mapambano dhidi ya Ukimwi pia limeamua kujikita katika vita dhidi ya Malaria.
|