24 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Viongozi nchini wametakiwa kuacha ubinafsi
 
2008-03-24 17:01:40
Na Radio One Habari

Viongozi wa serikali, mashirika ya umma na taasisi mbali mbali wamehimizwa kuacha ubinafsi na badala yake kuweka mbele maslahi ya umma kwa kuwahudumia kikamilifu wananchi.

Changamoto hiyo imetolewa na Askofu mstaafu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania-KKKT dayosisi ya Kaskazini Dr. Erasto Kweka.

Amesema mapiganao na machafuko yanayotokea mara kwa mara na kusababisha vifo vya wananchi wasio na hatia katika nchi nyingi husababishwa na ubinafsi wa viongozi tabia ambayo imeanza kujitokeza hapa nchini.

DR. Kweka alikuwa akizungumza wakati wa mazishi ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania katika nchi mbali mbali barani Afrika Marehemu Charles Kileo yaliyofanyika kijijini kwake mkuu Machame.

Wakati wa mazishi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete marehemu alitajwa kama kiongozi wa kuigwa katika kulitumikia taifa kwa uaminifu mkubwa aliouonyesha wakati wa uhai wake.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.