|
RUPOFA walaani tabia ya kuchanganya mafuta ya alizeti na mafuta mengine
2008-03-27 17:51:54
Na Radio One Habari
Chama cha wasindikaji cha mkoa wa Rukwa-RUPOFA kimelaani tabia iliyozuka miongoni mwa wasindikaji wa mafuta ya alizeti katika Manispaa ya Sumbawanga ya kuyachanganya na mafuta ya aina nyingine.
Mwenyekiti wa Chama hicho Bibi Rosalie Mwanakulya amesema tabia hiyo ipigwe vita kwa nguvu zote kwani inahatarisha afya na maisha ya watu wasiokuwa na hatia.
Ametoa shutuma hizo kwenye warsha ya wadau wa ujasiriamali wa mkoa huo wa Rukwa mjini Sumbawanga iliyoandaliwa na Shirika la Viwango nchini-TBS, kuhusu ubora wa bidhaa
Bibi Mwanakulya amesema wasindikaji hao wasiokuwa waaminifu wanachanganya mafuta ya alizeti na mafuta mengine yanayotengenezwa nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na ya aina ya Korie na dawa ya kuumulia unga wa maandazi na kisha kukamuliwa na malimao ili mafuta hayo yawe kama alizeti na yasiyoganda.
|