|
Mfuko wa Bima ya Afya kujenga hospitali kubwa Dar
2008-05-04 23:15:52
Na Radio One Habari
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unakusudia kujenga hospitali kubwa jijini Dar es Salaam ili kutoa huduma za matibabu na za uchunguzi kwa wanachama wa mfuko huo na wananchi wengine.
Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bwana Emanuel Humba imesema hospitali hiyo itatoa matibabu ya Daraja la kwanza na itakuwa na huduma zote muhimu.
Bwana Humba amesema kwa sasa Mfuko wake unawasiliana na mamlaka mbali mbali za Serikali pamoja na wadau wengine ili kupata eneo kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo, uamuzi ambao tayari umesharidhiwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko huo.
Hivi karibuni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ulitoa Shilingi Milioni 255 kwa ajili ya kukarabati sehemu za kutolea huduma katika hospitali za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Temeke, ikiwa ni juhudi za Mfuko huo kuboresha huduma za matibabu Jijini Dar es Salaam.
|