04 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Shilingi Milioni 10.8 za kujenga nyumba za walimu Kigoma hazikufanyakazi
 
2008-05-04 23:16:29
Na Radio One Habari

Shilingi Milioni 10.8 zilizokusudiwa kutumika katika ujenzi wa nyumba tatu za walimu wa shule ya msingi Rukoma katika halmashauri ya wilaya Kigoma hazikufanyakazi hiyo.

Hayo yameelezwa na Kamati ya Elimu, Afya na Maji ya halmashauri hiyo katika taarifa yake ambayo imebaini kuwa fedha hazikufanya kazi iliyotarajiwa.

Habari kutoka Kigoma zinasema kutokana na kuwepo kwa ujenzi hewa, taarifa nyingine za uhakika zimeeleza kuwa halmashauri ilikuwa ikitoa pesa kwa ajili ya ujenzi katika shule ya msingi Mwese ambayo iko wilayani Mpanda mkoani Rukwa.

Mbali na hilo, shule tatu hewa pia zimeonekana kujengwa katika kata ya Sigunga huku ripoti zikionesha kuwa shule hizo zimekamilika.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.