04 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Korogwe walaumiwa kwa kutochangia elimu
 
2008-05-04 23:17:02
Na Radio One Habari

Uongozi Wilayani Korogwe Mkoani Tanga umewalaumu baadhi ya wazazi wilayani humo kwa kushindwa kuchangia gharama za elimu na badala yake wamekuwa wakitegemea wahisani kuwatatulia matatizo yao.

Lawama hizo zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bibi Betty Mkwasa wakati wa uzinduzi wa miradi mbalimbali.

Miradi hiyo ni ya maji, majengo ya vyoo pamoja na shughuli ya upandaji miti lililofanywa na Shirika la Misaada la Marekani -USAID, kampuni ya Coca Cola pamoja na Shirika la World Visionna kughasrimu jumla ya Shilingi Milioni 26 katika shule ya msingi na sekondari ya mji mdogo wa Hale.

Bibi Betty Mkwasa amesema baadhi ya wazazi wamejenga dhana potofu kwamba hata milango na madirisha ya madarasa wanategemea wahisani au serikali wakati jukumu hilo lipo ndani ya uwezo wao.

Mapema wawakilishi wa wahisani Bwana Jeremiah Dafa wa Programu ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ya Pwani na Meneja wa Uhamasishaji wa World Vision Bwana Kuhanda Amitari wamesema miradi hiyo ni muhimu na inapaswa kuendelezwa.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.