|
Wanahabari tumieni uhuru wenu kuelimisha jamii
2008-05-04 23:18:04
Na Radio One Habari
Wanahabari na vyombo vya habari nchini wametakiwa kutumia uhuru waliopewa kisheria ili kueleza mambo muhimu yanayogusa jamii kwa lengo la kuharakisha maendeleo.
Naibu Waziri kiongozi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamuhuna amesema kuna umuhimu kwa vyombo vya habari kuandika zaidi juu ya mambo yanayowagusa wananchi yawe ya mafanikio au ya matatizo.
Mheshimiwa Shamuhuna ambaye pia ni Waziri wa Habari na Utamaduni amesema ni vyema kwa vyombo vya habari kuandika na kutayarisha vipindi juu ya uchumi, maendeleo katika sekta ya afya na shughuli nyenginezo za maendeleo ya kijamii kama mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Mheshimiwa Shamuhuna alikuwa akifungua majadiliano ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yaliyofanyika mjini Zanzibar.
Katika mada yake katibu mtendaji wa tume ya utangazaji Zanzibar Bwana Ali Mwinyikai alisema nchi ilikuwa inapita katika mageuzi ambayo wanahabari wanalazimika kuwa na majukumu ya ziada kusaidia jamii kupiga hatua za maendeleo.
|