07 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Vijana Kyela waishi kwa hofu ya kulazimishwa kuoa wajane
 
2008-05-07 19:36:01
Na Radio One Habari

Baadhi ya wananchi wilayani Kyela wamesema vijana wanaishi kwa hofu ya kupoteza maisha na wengine wamezikimbia familia zao kupinga kulazimishwa kurithi wajane.

Wananchi hao wamesema hayo katika mazungumzo na Radio One Stereo wakati wa mkutano uliozungumzia uzazi salama ulioandaliwa na Shirika la Huduma kwa Makazi na watu.

Wamesema pamoja na wanaharakati kupiga vita mila hizo, baadhi ya watu wanaziendeleza na kwamba vijana wanaojaribu kukataa vitendo hivyo, huugua ama kupoteza maisha.

Nao Meneja wa Mpango wa Uzazi Salama-PSI kanda ya Kusini Bwana Angelus Mhelela na Mkuu wa wilaya hiyo Bwana Mashimba Husein Mashimba wamesema elimu imeanza kutolewa kupiga vita mila hiyo ambayo inahatarisha maisha kwa walengwa na kuchangia uzazi usiozingatia mpango.

Wamesema baadhi ya wazazi kwa makusudi wanawakatisha masomo watoto wao, ili kuepuka mzigo wa kusomesha kutokana na kuzidiwa na idadi kubwa ya watoto.

  • SOURCE: Radio One
Tuma Maoni Yako
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.