08 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Serikali imeombwa kukabiliana na wimbi la waganga wa jadi
 
2008-05-08 14:34:44
Na Radio One Habari

Chama cha Waganga wa Tiba za Jadi nchini kimeiomba serikali na wadau wengine kusaidia kukabiliana na wimbi la baadhi ya waganga wa jadi wanaojihusisha na vitendo vinavyochochea mauaji ya binadamu.

Changamoto hiyo imetolewa mjini Arusha na Katibu wa chama hicho nchini Bwana Nyaki Huseini alipokuwa akizungumzia tukio la mganga wa jadi Bwana Juma Bakari Kimbunga aliyekamatwa na fuvu la kichwa cha binadamu mkoani humo.

Amesema pamoja na chama chao kuanza kampeni ya kuwasaka waganga hao wanaoharibu sifa ya taaluma yao, wanahitaji msaada wa wadau wengine na ameongeza kwamba wanaotumia viungo vya binadamu sio waganga bali ni wachawi.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Bwana Basilio Matei amesema polisi mkoani humo wameshaanza kukabiliana na tatizo la baadhi ya waganga wa jadi wanaochochea mauaji , ikiwa ni pamoja na kuwatambua waganga wote wa jadi wanaoendesha shughuli hizo.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.