08 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ongezeko la uhalifu linachangiwa na wafungwa walioachiwa kwa msamaha wa Rais
 
2008-05-08 14:36:11
Na Radio One Habari

Ongezeko la sasa la uhalifu mkoani Kilimanjaro linachangiwa na wafungwa walioachiwa kwa msamaha wa Rais Jakaya kikwete wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 44 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kilimanjaro Bwana Lucas Ng`hoboko amewaambia waandishi wa habari kuwa wafungwa hao wanatumia silaha zao walizozificha kufanya uhalifu baada ya kuachiwa huru kwa msamaha wa rais.

Ametaja sababu nyingine kuwa ni kushuka kwa uzalishaji katika migodi ya Merarani, hali inayowafanya wachimbaji kuachana na kazi hiyo na kujiingiza katika uhalifu.

Aidha amesema kuzorota kwa shughuli za utalii katika hifadhi ya mlima Kilimanjaro wakati huu kumeathiri kipato cha wengi wakiwamo wahalifu walioacha uhalifu na kuwapandisha mizigo ya watalii mlimani na kujipatia kipato.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.