|
Wananchi waliokuwa wakiishi karibu na mlima Oldonyo Lengai warejea katika makazi yao
2008-05-08 14:36:59
Na Radio One Habari
Wananchi waliokuwa wakiishi karibu na mlima Oldonyo Lengai wilayani Ngorongoro ambao waliyakimbia makazi yao kutokana na kulipuka kwa volcano katika mlima huo, wameanza kurejea katika makazi yao.
Hali hiyo imetokana na kutoweka kwa uwezekano wa volcano hiyo kulipuka tena.
Wakizungumzia uamuzi wao wa kurudi tena karibu na mlima huo wananchi hao wamesema maelezo yanayotolewa na serikali na wataalam wake ya kuwataka kukaa mbali na mlima huo hayajitoshelezi na kwamba hayalingani na hali halisi.
Hata hivyo, Mkuu wa wilaya Ngorongoro Bwana Jowika Kasunga amekanusha uvumi ulioenea kwa wananchi hao kuwa nia hiyo ya serikali ni njama za kutaka kuwapora wananchi ardhi yao na kuwapa wawekezaji.
|